International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa January 24 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Jan 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa January 24 2025

Chelsea wanafikiria kumsajili winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, baada ya Napoli kusitisha mpango wa kusajilia mchezaji huyo wa Manchester United. (Sky Sports)

Manchester City inavutiwa na beki wa Italia Andrea Cambiaso, 24, lakini Juventus inataka euro milioni 65. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Borussia Dortmund wamejiondoa katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, huku mshahara wa mchezaji huyo wa Manchester United wa pauni 350,000 kwa wiki ukionekana kikwazo. (Mail)

Beki wa Arsenal na Ukraine Oleksandr Zinchenko, 28, anatarajiwa kuondoka kabla ya dirisha la uhamisho wa Januari kufungwa, huku Borussia Dortmund wakimkamia. (Telegraph)

Dortmund pia inamfuatilia beki wa Chelsea na England Ben Chilwell, 28, kama chaguo mbadala. (Sun)

Chelsea imefikia makubaliano ya awali ya kumtoa kwa mkopo kiungo wa Ureno Renato Veiga, 21, kwenda Juventus kwa muda uliosalia. (Athletics)

Beki wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 27, yuko mbioni kusaini mkataba wa awali wa kurejea Celtic kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)

West Ham wanamtaka mchezaji wa RB Leipzig Andre Silva, 29, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu lakini watamchukua mshambuliaji wa Ajax na Uholanzi Brian Brobbey, 22, ikiwa watashindwa kufikia dili la kumsajili mshambulizi huyo wa Ureno. (Florian Plettenberg)

West Ham wanamfuatilia kiungo wa Uingereza Dan Neil lakini Sunderland wanasita kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuondoka katika msimu huu wa usajili wa wachezaji. (Guardian)

Aston Villa wanataka kusajili mlinzi wa Ufaransa Loic Bade, 24, kutoka Sevilla baada ya kumruhusu beki wa Brazil Diego Carlos, 31, kusajiliwa na Fenerbache. (Express and Star)

Chelsea inamnyatia kiungo wa Hellas Verona na Morocco Reda Belahyane, 20, huku wakijiandaa kummuuza mchezaji wa Italia Cesare Casadei, 22. (Gianluca di Marzio - kwa Kiitaliano)

Beki wa Jamhuri ya Ireland Andrew Omobamidele, 22, anakaribia kuhamia klabu ya Ufaransa ya Strasbourg kutoka Nottingham Forest. (Athletics)

Wolves wamekataa ofa ya awali ya Millwall kwa ajili ya kiungo wa kati wa Uingereza Luke Cundle, 22, ambaye pia anasakwa na Swansea na Bristol City. (Express and Star)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’