Klabu ya Simba imewaombea uraia wa Tanzania wachezaji wake 9 wa kigeni ambao hawaitwi katika timu zao za Taifa, imefahamika
Hatua imekuja siku chache baada ya klabu ya Singida Black Stars kufanikisha kupata uraia wa Tanzania kwa wachezaji wao wanne, Emmanuel Keyekeh (27) kutoka Ghana, Arthur Bada (22) kutoka Ivory Coast, Amas Obasogie (22) kutoka Nigeria na Damaro Camara (21) kutoka Guinea
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amethibitisha timu hiyo kupeleka maombi hayo Uhamiaji pia wakiomba kupewa utaratibu ili kufanikisha jambo hilo
"Ni kweli Simba imetuma maombi Idara ya uhamiaji kuomba wachezaji 9 wa Kimataifa ambao hawapati nafasi katika timu zao za Taifa ili wapewe uraia wa Tanzania. Kinachosubiriwa ni maelekezo kutoka Uhamiaji ili mchakato huo uanze mara moja," alisema Ahmed
Breaking News..!!
β Bin Kazumari (@jemedarisaid) January 23, 2025
Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imeandika barua kwa Kamishina Jenerali wa Uhamiaji nchini ikiwaombea uraia wa Tanzania wachezaji wake 9 Kati ya 12 ambao imewasijili kwa mujibu wa kanuni za ligi Kuu ya bara. Ngoma ndo kwanza imeanza sasa, fungeni vibwebwe! pic.twitter.com/qPMbF14nPW



