Local,Normal News,Pamba

Pamba yaacha sita dirisha dogo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Jan 2025
Pamba yaacha sita dirisha dogo

Bado Klabu ya Pamba Jiji inaumiza kichwa namna ya kumalizana na mshambuliaji, Mghana Erick Okutu ambaye mwanzo ilielezwa angejiunga na KenGold dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15, mwaka huu, lakini imeshindikana

Wakati ishu ya Okutu ikiwa pasua kichwa, klabu hiyo imeachana na nyota sita kipindi cha dirisha dogo

Inaelezwa kambi ya Okutu haikukubaliana na uamuzi wa mteja wao kutolewa kwa mkopo, isipokuwa kwa sharti moja la kuuvunja mkataba uliobaki wa miezi sita

Okutu alinukuliwa akisema hana taarifa za kutolewa kwa mkopo kwani anachokifahamu bado ana mkataba wa miezi sita na kikosi hicho, huku akiweka wazi hana dhamira yoyote ya kuondoka labda itokee ofa kwa timu nyingine kutoka nje

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Pamba Jiji, Ezekiel Ntibikeha, alisema klabu hiyo imekubali kukaa mezani na mchezaji huyo ili kupata muafaka wa namna ya kuvunja mkataba wake baada ya maingizo mapya dirisha dogo

"Okutu tulikuwa na mpango wa kumpeleka kwa mkopo KenGold lakini mwishoni kabisa wenzetu wakaukataa ule uhamisho, tumeamua kukaa naye mezani tupate mwafaka lakini tutakuwa kwenye mazingira mazuri ya kumalizana naye," alisema Ntibikeha

Ntibikeha ambaye pia ni meneja wa Pamba Jiji, alisema kuwa katika dirisha dogo wamesajili wachezaji tisa na kuacha sita wakiwemo watatu waliopelekwa timu nyingine kwa mkopo akiwemo George Mpole aliyetimkia Kagera Sugar

Aliwataja walioachwa ni John Mtobesya, Emmanuel Boateng (Ghana), Robert Kouyala (Togo) na Salim Kipemba

"Tumemalizana nao kabisa baada ya kuona mwalimu ametoa mapendekezo yake na sisi tumejiridhisha ni kweli hawajapata nafasi kwa mechi 16 zilizopita, tukaona yawezekana kwa mechi hizi zinazofuata hatuwezi kuwatumia kwahiyo tulikaa nao mezani na kumalizana," alisema Ntibikeha

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’