Local,Normal News,

Karia njia nyeupe CAF

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Jan 2025
Karia njia nyeupe CAF

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), wamempitisha Rais wa baraza hilo, Wallace Karia, kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)

Uchaguzi Mkuu wa CAF unatarajiwa kufanyika Machi, mwaka huu nchini Morocco. Karia, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), alikuwa anatarajia kuchuana na Rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Moses Magogo

"Magogo hatagombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya CAF na sasa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia atakuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo. maana yake tayari Karia ameshapita katika nafasi hiyo," chanzo chetu kilisema

Karia pia amethibitishwa kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao wa TFF, utakaofanyika baadaye mwaka huu

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, waliazimia hivyo katika mkutano wa mwaka uliofanyika Desemba 21, mwaka jana mkoani Kilimanjaro

CECAFA pia imetangaza kumuunga mkono Rais wa Shirikisho la Soka la Djibouti, Souleiman Waberi, kuwania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji wa FIFA, ambayo pia itafanya uchaguzi wake baadaye mwaka huu. Waberi, mwamuzi wa zamani wa kimataifa, kwa sasa ni Makamu wa Tatu wa Rais wa CAF

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’