Local,Normal News,Yanga

Ramovic afafanua kauli kuhusu Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Jan 2025
Ramovic afafanua kauli kuhusu Ligi Kuu

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema hawakuwa na bahati kufuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa lakini sasa wanafanya kazi kubwa katika uwanja wa mazoezi ili kujiimarisha na kuwa bora zaidi

Akizungumza baada ya mchezo wa CRDB Cup dhidi ya Copco Fc jana ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 5-0, Ramovic aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo na pia akazungumzia kwa ufupi nini anafanya katika uwanja wa mazoezi ili Yanga iendelee kucheza kwa kasi na ari kubwa

"Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu, matokeo haya ni mwendelezo wa dhamira yetu ya kucheza aina ya soka la ushindani lenye 'intensity' ya juu"

"Tunafanya mazoezi ya kukimbia na kuimarisha utimamu wa wachezaji wetu ili kuhakikisha wanacheza aina hii ya soka"

"Baada ya kutolewa katika ligi ya mabingwa nilisema kuhusu wachezaji wangu kukosa utimamu wa kucheza aina hii ya soka bahati mbaya baadhi ya waandishi wa habari hawakunielewa wakasema naidharau ligi ya Tanzania jambo ambalo si kweli"

"Mimi nilikuwa nazungumzia timu yangu ya Yanga na kile tunapaswa kuboresha ili kuwa na ushindani katika ligi ya mabingwa"

"Lengo langu ni kuona Yanga inaweza kucheza nusu fainali na hata kutwaa taji la ligi ya mabingwa. Naamini tuko katika njia sahihi na tutafikia malengo yetu," alisema Ramovic

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’