Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Fountain Gate, Singida BS

Droo Afcon 2025 ni leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Jan 2025
Droo Afcon 2025 ni leo

Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', itajua wapinzani wake itakaokutana nao wakati droo ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), itakapofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mohammed V uliopo Rabat jijini Morocco

Stars ni kati ya timu 24 zitakazoshiriki michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi Morocco kuanzia Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18 mwakani, ikiwa ni AFCON ya 35, kufanyika katika historia tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 1957

Timu 24 zilizofuzu zitapangwa katika vyungu vinne vyenye timu sita kulingana na ubora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ambapo Stars iko chungu cha nne na wawakilishi wengine wakiwamo, Msumbiji, Comoro, Zimbabwe, Sudan na Botswana

Chungu cha kwanza kitakuwa na wenyeji Morocco, Senegal, Misri, Algeria, Nigeria na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Ivory Coast, huku kile cha pili kikiwa na timu za Cameroon, Mali, Tunisia, Afrika Kusini, DR Congo na Burkina Faso

Chungu cha tatu kinaundwa na Gabon, Angola, Zambia, Uganda, Equatorial Guinea na Benin ambapo katika droo hiyo kutakuwa na makundi sita yenye timu nne, huku zitakazomaliza katika nafasi mbili za juu kwa kila kundi zitafuzu moja kwa moja hatua ya 16

Timu hizo zitaungana na nne zitakazomaliza katika nafasi ya tatu zikiwa na matokeo bora zaidi ili kukamilisha idadi ya timu 16, ambazo zitaanza kushindania taji hilo kubwa Barani Afrika, ambalo litachezwa kwenye viwanja sita vilivyopo katika majiji sita

Stars ilikata tiketi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ya Kundi H ikiwa na pointi 10, nyuma ya DR Congo iliyomaliza na pointi 12, huku Guinea ikishika ya tatu na pointi tisa, wakati Ethiopia ilimaliza na pointi nne

AFCON ya mwaka huu ni ya nne kwa Stars katika historia yake ambapo mara ya kwanza ilikuwa ya Nigeria mwaka 1980, kisha ikashiriki tena baada ya miaka 39, ilipofanya hivyo mwaka 2019, Misri chini ya kocha mkuu, Mnigeria Emmanuel Amuneke

Mwaka huu imefuzu kwa mara ya nne tena ikijiwekea rekodi ya kipekee baada ya kufuzu ikiwa chini ya kocha mzawa, Hemed Suleiman 'Morocco', kwani kabla ya hapo haikuwahi kutokea

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’