Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu Afrika (ACA) Injinia Hersi Said leo atatia saini makubaliano na uzinduzi wa ofisi ya Makao Makuu ya ACA katika hafla maalum itakayofanyika Rabat, Morocco
Ofisi ya ACA itakuwa katika Jengo la Mohammed VI De Football, jengo ambalo pia kuna ofisi za Shirikisho la soka Duniani (FIFA)
Katika jengo hilo pia kutakuwa na ofisi ndogo za CAF kwaajili ya michuano ya AFCON 2025 itakayofanyika baadae mwaka huu huko Morocco