Local,Normal News,Singida

Pluijm aitabiria makubwa Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Jan 2025
Pluijm aitabiria makubwa Singida BS

Kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm amesema kutua katika Ligi Kuu Bara kwa majina ya nyota wa kimataifa akiwamo Jonathan Sowah na Serge Pokou katika kikosi cha Singida Black Stars kutakiimarisha kikosi hicho.

Pluijm alisema amekua akiifuatilia Ligi Kuu Bara na naamini ndani ya misimu miwili au mitatu ijayo Singida Black Stars inaweza kuwa moja ya timu tishio kutokana na uwekezaji inaoufanya.

Pluijm aliyewahi kuifundisha Singida United kabla ya kutua Azam FC, alisema Singida imeonyesha uthubutu kufanya usajili mkubwa tangu mwanzo mwa msimu na miongoni mwa majina yaliyomshtua ni pamoja na Sowah na Pokou.

Licha ya kuwa na Elvis Rupia ambaye ni kinara wa mabao Ligi Kuu, Singida BS ilimuongeza katika dirisha lililopita Sowah (pichani) ambaye ni mmoja wa washambuliaji hatari kutoka Al-Nasr ya Libya aliyekuwa pia akimezewa mate Yanga.

"Inapendeza kuona timu nyingine zikiibuka na kuonyesha kuwa zinaweza kushindana, kikubwa ni kuendelea kuamini katika mipango yao, kiukweli kama ubora wa wachezaji nimeuona ni mkubwa"

"Inatakiwa kuwepo kwa timu nyingine tatu hadi nne kama Singida. Uwepo wake utafanya ligi ya Tanzania kuendelea kukua na ushindani utakuwa mkubwa zaidi," alisema Pluijm

Kocha huyo alieleza awali alijipa muda kuwatazama Singida kuona kile walifanya katika michezo ya mwanzoni mwa msimu lakini wamethibitisha kuwa wanaweza kupambania nafasi za juu.

Kwa sasa Singida ipo nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 33 kupitia michezo 16, pointi mbili pungufu na ilizonazo Azam iliyopo nafasi ya tatu ikimiliki 36 na sita pungufu na zile za Yanga yenye 39, wakati Simba inaongoza ikiwa na 40

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’