Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Januari 29 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Jan 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Januari 29 2025

Roma wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United na Brazil Casemiro, 32, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu, lakini uhamisho unategemea kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Argentina Leandro Paredes, 30. (Mail)

Napoli na Juventus wanamfuatilia mshambuliaji wa Manchester United Rasmus Hojlund, 21, huku mshambuliaji huyo wa Denmark akiwa bado hajamvutia kocha mpya Ruben Amorim. (Sportsport)

Al-Hilal wamepewa nafasi kubwa ya kumsajili winga wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah, 32, msimu huu baada ya timu hiyo ya Saudi Pro League kughairi kandarasi ya fowadi wa Brazil Neymar, 32. (Telegraph – Subscription Required)

Wolves wanatarajia ofa moja au zaidi kwa fowadi wa Brazil Matheus Cunha kabla ya tarehe ya mwisho ya dirisha la uhamisho, huku Aston Villa, Arsenal na Nottingham Forest wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)

Manchester United wanakaribia kumsajili winga wa Lecce na Denmark Patrick Dorgu, 20, kwa ada ya pauni milioni 30. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 27, ameamujiri kaka yake mshambuliaji wa Brighton Danny Welbeck kama wakala wake mpya ili kumsaidia kupata uhamisho kutoka Old Trafford. (Star)

Kwa hali ilivyo, chaguo pekee la Rashford kuondoka United mwezi huu litakuwa ni uhamisho wa mkopo kwenda Juventus. (Independence)

Mshambulizi wa Bayern Munich na Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Mathys Tel, 19, anataka kuondoka katika klabu hiyo mwezi huu na Chelsea wako kwenye mazungumzo na timu hiyo ya Bundesliga. (Mail)

Manchester United pia itaingia kwenye kinyang'anyiro cha kumuwania Tel lakini iwapo tu Rashford au winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, watauzwa. (Florian Plettenberg)

Kiungo wa kati wa Manchester City James McAtee, 22, hauzwi tena na Bayer Leverkusen, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikipanga kumsajili mchezaji wa Argentina Emiliano Buendia, 28, kutoka Aston Villa. (Florian Plettenberg)

Manchester City wanakabiliwa na kinyang'anyiro cha kuwania saini ya Andrea Cambiaso, 24, kwani Juventus watafanya uamuzi wa mwisho tu kuhusu mustakabali wa beki huyo wa pembeni wa Italia baada ya mechi ya Jumatano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica. (Nipe Sport)

Bayern Munich na Manchester United wana nia ya kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Christopher Nkunku, 27, ambaye thamani yake ni takriban £70m. (Mail)

Manchester City wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Brazil Douglas Luiz, 26, kwa mkopo, lakini klabu hiyo ya Serie A inataka kuingiza kipengele cha wajibu wa kununua katika mkataba wowote wa muda. (Mail)

Brighton wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa wiki ijayo.(Athletic - subscription required)

Bayer Leverkusen wapo kwenye mazungumzo na Brighton ili kumsajili Ferguson. (Sky Sports)

Mshambulizi wa Leverkusen na Nigeria Victor Boniface, 24, aliondolewa mazoezini Jumanne huku kukiwa na uwezekano wa kuhamia Al-Nassr. (Athletic – Subscription Required)

Liverpool watamrejesha kiungo wa kati wa Uhispania chini ya umri wa miaka 21 Stefan Bajcetic kutoka kwa kipindi chake cha mkopo katika klabu ya Red Bull Salzburg na kumpeleka mchezaji huyo wa miaka 20 Las Palmas kwa msimu uliosalia. (Atlantico; In Spanish)

Wolves wako kwenye mazungumzo na Ajax kuhusu kusitisha mkopo wa winga wa Ureno Carlos Forbs, 20. (Athletic – Subscription Required)

Sheffield Wednesday wamewasilisha ofa ya mkopo kwa beki wa Ipswich Town mwenye umri wa miaka 23 Harry Clarke. (Sheffield Star)

Udinese wana nia ya kumsajili kipa wa Southampton na Jamhuri ya Ireland Gavin Bazunu, 22, kwa mkopo. (Ireland – Independence – Subscription Required)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
19m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’