Local,Normal News,Simba, Tabora

Ahmed atamba, Tabora United wataumia Jumapili

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Jan 2025
Ahmed atamba, Tabora United wataumia Jumapili

Kikosi cha Simba kitaelekea mkoani Tabora Jumamosi ya Februari 1 tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United utakaopigwa Jumapili, Februari 02 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema tayari timu imerejea mazoezini kujiandaa na mchezo huo mgumu lakini muhimu kwa Simba kushinda ili kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi

Ahmed amesema Simba inatambua ugumu wa mchezo huo hasa ikizingatiwa Tabora United walizifunga timu nyingine shindani

"Timu imerejea mazoezini baada ya mchezo wa kombe la CRDB dhidi ya Kilimanjaro Wonders. Wachezaji wote wamerejea ikiwa ni pamoja na wale waliokuwa wamepewa mapumziko na wengine kupewa ruhusa kusafiri nje ya nchi kuona familia zao"

"Timu itaondoka Dar es salaam siku ya Jumamosi, Februari 1 kuelekea Tabora kwa ajili ya mchezo dhidi ya Tabora United utakaopigwa Jumapili, Februari 2"

"Tunatambua hautakuwa mchezo mwepesi kwani Tabora United wameimarika sana ukilinganisha na tulivyocheza nao mara ya kwanza na kuwafunga mabao 4-0"

"Wamepata ushindi dhidi ya timu zinazoshika nafasi ya pili na tatu, hivyo wanaona kama wanaweza kuifunga Simba pia"

"Lakini niwaambie Simba ni timu tofauti na imara zaidi kuliko hizo timu walizozifunga na ndio maana iko kileleni mwa msimamo wa ligi. Hivyo sisi tutakwenda Tabora tukiwa na matumaini makubwa ya kushinda siku ya Jumapili," alisema Ahmed

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’