Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania Baraka Majogoro ameachana na klabu yake ya Chippa United kwa makubaliano ya pande zote mbili
Majogoro (27) alijiunga na klabu hiyo ya Afrika Kusini Agosti 2023 akisaini mkataba wa miaka minne ambao ungemuweka katika timu hiyo hadi 2027
Nyota huyo wa zamani wa klabu ya KMC kwa sasa ni mchezaji huru, mkataba wake uliosalia ukivunjwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili
Dirisha la usajili Afrika Kusini limefungwa, huenda nyota huyo akalazimika kusubiri hadi mwezi Julai kujiunga na timu mpya