Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Februari 03 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Feb 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Februari 03 2025

Mshambuliaji wa Ufaransa Mathys Tel, 19, anataka kujiunga na Manchester United lakini mazungumzo ya kufanikisha azama hiyo na Bayern Munich yametibuka kwa sasa, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka aondoke uhamisho wa kudumu. (Sky Germany)

Manchester United wanamtaka Tel, lakini mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Christopher Nkunku, 27, ni chaguo jingine katika siku ya mwisho. (ESPN)

Arsenal wanasubiri kwa hamu baada ya ofa mbili zilizowasilishwa na United kumsajili Tel kukataliwa siku ya Jumapili. (Mail)

Tottenham wamekubali Chelsea kumsajili mkataba wa mkopo na mlinzi Axel Disasi, 26, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anataka kuhamia Aston Villa. (Fabrizio Romano)

Beki wa kushoto wa Chelsea na England Ben Chilwell, 28, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Crystal Palace, kabla ya kuhamia klabu hiyo kwa mkopo siku ya mwisho wa uhamisho wa wachezaji. (Telegraph - usajili unahitajika)

Newcastle itamruhusu mlinzi wa Uingereza Lloyd Kelly, 26, kuelekea Juventus katika mkataba ambao utafanywa wa kudumu msimu wa joto. (Mail)

Joao Felix anatarajia kuondoka Chelsea siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji huku klabu za AC Milan na Aston Villa zikiwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 25. (Sky Germany)

Manchester United wamejitosa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ipswich na England wa Chini ya miaka 21 Liam Delap, 21, ambaye pia amekuwa akihusishwa na nklabu ya Tottenham. (Express)

Ajax haitamruhusu kiungo wa Uingereza Jordan Henderson, 34, kuhamia Monaco kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji. (Mail)

Everton wanashughulikia mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Rennes na Ufaransa Adrien Truffert, 23. (Mail)

Mkufunzi wa Crystal Palace Oliver Glasner anataka kumsajili kiungo wa AC Milan na Serbia Strahinja Pavlovic, 23, kwa mkataba wa pauni milioni 25. (Sun)

Kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Italia Jorginho, 33, anakaribia kufikia mkataba wa kujiunga na klabu ya Brazil Flamengo msimu wa joto. (Sky Italy, via Sky Sports)

Spurs wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Lorient Mfaransa Eli Junior Kroupi, 18, ambaye pia anawindwa na Chelsea na West Ham. (Football Insider)

Brighton wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa PAOK wa Ugiriki Stefanos Tzimas, 19, ambaye Nurnberg yuko kwa mkopo . (Sky Sports)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
1h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
3h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
4h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
6h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’