International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Februari 06 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Feb 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Februari 06 2025

Arsenal wako tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho msimu wa kiangazi kwa dau la £100m (euro 120m) kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, mwenye umri wa miaka 27. (Fichajes - In Spanish)

Mshambulizi wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21, anasalia kuwa nambari tisa katika orodha ya wachezaji ambao Arsenal ina uwezekano mkubwa wa kuwasajili msimu katika msimu huu wa kiangazi huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa na uwezekano mkubwa wa kumpiga bei katika uhamisho wake. (Independent)

Arsenal pia ilifanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa AC Milan na Uhispania Alvaro Morata, 32, wiki iliyopita kabla ya kujiunga na Galatasaray kwa mkopo. (Subscription reguired)

Manchester City wako tayari kushindana na Real Madrid kwa ajili ya kumnunua beki wa kushoto wa AC Milan Mfaransa Theo Hernandez, 27, iwapo watamkosa beki wa Juventus na Italia Andrea Cambiaso, 24 . (TeamTalk)

Kipengele cha kutolewa katika mkataba wa mshambuliaji wa Bayern Munich na England Harry Kane, 31, kitapungua kutoka £67m hadi £54m katika mwaka ujao. (BILD - Subscription reguired)

Mkufunzi wa Chelsea Enzo Maresca anapanga kumtumia kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos mwenye umri wa miaka 20 ambaye kwa sasa yuko Strasbourg kwa mkopo katika kikosi chake cha kwanza msimu ujao. (Fabrizio Romano)

Arsenal itatafuta kumsajili mlinda mlango wa Uhispania Joan Garcia, 23, kutoka Espanyol msimu wa kiangazi. (Subscription required)

Chelsea ilishindwa katika jaribio jaribilo lake la kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Tottenham Mfaransa Mathys Tel, 19, kutoka Bayern Munich siku ya makataa. (L'Equipe -in France)

Beki wa kushoto wa Manchester United na Uholanzi Tyrell Malacia, 25, angejiunga na Wolves siku ya mwisho, lakini akachagua PSV Eindhoven badala yake. (Voetbal Verslaafd - in Dutch)

Mmoja wa wachezaji wanne waliosajiliwa na Manchester City Januari atakosa mechi yao ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid kwasababu sheria za Uefa zinaruhusu wachezaji watatu pekee waliosajiliwa kuongezwa kwenye orodha ya kikosi kabla ya hatua ya mtoano. (ESPN)

Napoli walikatisha nia yao ya kumnunua winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 20, kwasababu alidai mshahara mkubwa sana. (Fabrizio Romano)

Iwapo klabu itaanzisha kipengele cha kutolewa kwa Kane katika klabu ya Bayern Munich basi klabu yake ya zamani Tottenham Hotspur italazimika kuamua kama itatimiza ofa hiyo na angependelea kurejea London Kaskazini. (Telegraph - Subscription reguired)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’