Kikosi cha Simba jioni ya leo kitashuka uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara kumenyana na Fountain Gate katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Simba iliwasili Manyara mapema jana na jioni kikosi kikafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa
Ni mechi nyingine kwa Simba kuzisaka alama zote tatu, matokeo ambayo yatawarudisha kileleni mwa msimamo wa ligi
Lakini ni wazi hawatakuwa na kazi nyepesi, Fountan Gate wamepata muda wa kujipanga zaidi huku wakifanya maboresho kadhaa katika dirisha dogo ikiwa ni pamoja na kuleta kocha mpya
Timu hizo zilipokutana katika duru ya kwanza uwanja wa KMC Complex, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0
Mechi nyingine zinazopigwa leo;
