Local,Normal News,Pamba, Azam, Namungo, Dodoma

Pamba yaiduwaza Azam Fc CCM Kirumba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Feb 2025
Pamba yaiduwaza Azam Fc CCM Kirumba

Jana Pamba Jiji waliiduwaza Azam Fc katika dimba la CCM Kirumba wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara

Bao lililowazamisha Azam FC lilifungwa na kiungo mkongwe, Deus David Kaseke dakika ya 86, akigusa mpira wa kwanza baada tu ya kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya kiungo Mrundi, Shassir Nahimana

Ushindi huo wa pili mfululizo wakitoka kushinda ugenini dhidi ya Dodoma Jiji 1-0 pia, umeifanya Pamba Jiji FC ifikishe pointi 18 katika mchezo wa 18 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 12, wakati Azam FC imbaki na pointi zake 39 za mechi 18 pia nafasi ya tatu

Katika mechi nyingine, wenyeji Namungo Fc walilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Dodoma Jiji katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi

Mabao ya Namungo Fc yalifungwa na Pius Buswita dakika y 44 na Erasto Nyoni dakika ya 56 kwa penalti, wakati ya Dodoma Jiji walitangulia kufunga mabao yao kupitia Paul Peter dakika ya 21 na Apollo Otieno dakika ya 31

Kwa matokeo hayo, Namungo Fc wamefikisha pointi 18 katika mchezo wa 18 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 13, wakati Dodoma Jiji wakifikisha pointi 20 katika mchezo wa 18 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya nane

Mechi nyingine tatu zinapigwa leo, Ken Gold itakuwa mwenyeji wa Fountain Gate huku KMC ikiumana na Singida BS na mechi nyingine kuwakutanisha JKT Tanzania dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’