Local,Normal News,Dodoma

Majeruhi wanaendelea vizuri - Dodoma Jiji

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Feb 2025
Majeruhi wanaendelea vizuri - Dodoma Jiji

Siku ya Jana tar. 10/02/2025 majira ya saa 4 asubuhi Kikosi chetu Kilichokua safarini kutokea Ruangwa Mkoani Lindi Kuelekea Jijini Dar es salaam kilipata ajali ya gari Mkoani Lindi kwa kupinduka na kutumbukia Mtoni (Mto Matandu)

Ajali hiyo ilisababisha majeruhi kadhaa akiwemo mwalimu wa viungo Francis Mkanula mshambuliaji wetu Yassin Mgaza pamoja na Rajab ambae ni golikipa wa timu yetu ya vijana chini ya Miaka 20, ambapo majeruhi wote walikimbizwa katika Kituo Cha Afya Nangurukuru kwa matibabu zaidi

Majeruhi wanaendelea vizuri na baada ya vipimo na matibabu ya awali waliruhusiwa na Kikosi chetu kiliendelea na safari na kimefanikiwa kufika Dar es salaam salama

Tunatoa shukrani kwa Wasamalia wema waliojitokeza kufanya uokoaji eneo la tukio, Madaktari pamoja na jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi kwa msaada na jitihada zote walizozifanya kuhakikisha kila kitu kinakua sawa

Aidha tunavishukuru vyombo vya habari, wanahabari na taasisi mbalimbali zinazoendelea kutuma salamu za pole na kututia moyo katika kipindi hiki kigumu

Tunawaombea Majeruhi wote wapone haraka ili waweze kurejea kwenye majukumu yao.

DODOMA JIJI FC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’