Local,Normal News,Yanga, JKT

Hamdi akubali droo dhidi ya JKT Tanzania

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Feb 2025
Hamdi akubali droo dhidi ya JKT Tanzania

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema matokeo ya suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania jana, hayawezi kuwaondoa katika mkakati wao wa kutetea ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Akikiongoza kikosi cha Yanga kwa mara ya kwanza akiwa kwenye benchi, Hamdi alishuhudia vijana wake wakikosa ushindi kwa mara ya kwanza ugenini msimu huu ikiwa pia ndio sare ya kwanza

Akizungumzia mchezo huo, Hamdi alisema malengo yao ilikuwa kuibuka na ushindi lakini unapokosa alama tatu, basi ni bora upate alama moja kuliko kukosa kabisa

Hamdi amesisitiza matokeo hayo haya-athiri mikakati yao katika mbio za ubingwa licha ya kuwa Yanga inaweza kushuka nafasi ya pili leo kama Simba itashinda dhidi ya Prisons

"Ilikuwa mechi ngumu, sio rahisi kucheza mechi ya aina hii ambayo mpinzani anakaa nyuma muda wote. Tulipoteza nafasi tatu adimu katika kipindi cha kwanza"

"Niseme tu washambuliaji wangu hawakuwa na bahati ya kuweka mpira nyavuni, wapinzani wetu walipata nafasi moja tu ya wazi, kwa asilimia 80 ya mchezo walikuwa wakizuia"

"Unapokosa alama tatu basi ni bora upate angalau alama moja, leo tumepata alama moja, tutajipanga kufanya vizuri katika mchezo ujao"

"Kwa uzoefu wangu hatupaswi kuhofia kuwa nafasi ya pili kwa sababu ni ngumu sana kudhibiti nafasi ya kwanza pale mnapochuana kuwania ubingwa," alisema Hamdi

Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya KMC utakaopigwa Ijumaa, Februari 14 katika dimba la KMC Complex

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
37m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’