Mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Wazir Jr Shentembo amejiunga na Al Mina'a FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Iraq akimfuata Simon Msuva anayekipiga katika timu ya Al Talaba.
Wazir Jr ambaye aliwahi kukipiga Yanga 2020/21, amesaini mkataba wa miezi sita kujiunga na timu hiyo iliyopo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 20.
Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fortunatus Johnson amesema nyota huyo amejiunga na timu hiyo kwa mkopo na mwisho wa msimu watakaa na kuangalia namna ya kuboresha maslahi yake kwa kuwa atarejea katika kikosi hicho.
"Timu hiyo ilimuona alipokwenda kufanya trial (majaribio) nchini Brunei ambako kulikuwa na mawakala mbalimbali, baada ya timu ya nchi hiyo kuchelewa (kumsajili) Mina'a ikamsajili," alisema
Junior alitambulishwa zaidi ya Toto Africa 2020/21 akifunga mabao 14 na baadae kusajiliwa na Yanga ambayo aliitumikia kwa misimu miwili kisha kujiunga naa KMC akiifungia mabao 13 2022/23