Yanga imeendeleza ubabe katika ligi kuu ya NBC ikiichapa KMC mabao 6-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Stephane Aziz Ki alikuwa shujaa wa Yangaa katika mchezo huo akifunga hat-trik na kubeba tuzo ya nyota wa mchezo
Mabao mengine ya Yanga katika mchezo huo ambao waliutawala kwa muda mwingi yalifungwa na Prince Dube, Maxi Nzengeli na Israel Mwenda
Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa KMC lilifungwa na Redemtus Mussa
Ushindi huo umeirejesha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 49
Katika mechi nyingine zilizopigwa leo, Tabora United ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ken Gold wakati Kagera Sugar ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate
Prisons wamepoteza mechi nyumbani kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Namungo Fc



