Kocha Mkuu wa Azam Fc Rachid Taoussi amesema kipigo dhidi ya Pamba Jiji kilimfanya akose usingizi kwa siku mbili huku akifanya vikao na wachezaji wake kuhakikisha hawarudii makosa waliyofanya katika mchezo huo
Leo Azam Fc itakuwa dimba la Azam Complex kuikabili Mashujaa Fc katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC
"Sijalala siku mbili kutokana na kupoteza mchezo dhidi ya Pamba Jiji. Nimefanya kikao na wachezaji tusije kufanya makosa kama tuliyofanya mechi iliyqopita na tuwe tayari kwa mchezo dhidi ya timu ngumu ya Mashujaa," alisema Taoussi
Kipigo dhidi ya Pamba Jiji kiliwapunguza kasi Azam Fc katika malengo yao ya kuwania ubingwa msimu huu
Pengine leo waanahitaji kushinda dhidi ya Mashujaa Fc ambayo imekuwa na mwendo wa kusuasua ikicheza mechi 6 bila ushindi
Mchezo mwingine unaopigwa leo, Pamba Jiji itakuwa mwenyeji wa Coastal Union uwanja wa CCM Kirumba