Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi za mzunguuko wa 20 zitaunguruma
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga, watakuwa uwanja wa nyumbani KMC Complex kumenyana na Singida Black Stars katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Mechi kati ya Yanga dhidi ya Singida Black Stars haijawahi kuwa nyepesi. Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa visiwani Zanzibar, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee likifungwa na Pacome Zouzoua
Singida BS wametoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, uwanja ambao Yanga ilidondosha alama mbili dhidi ya maafande hao
Lakini pia Wananchi wametoka kuichabanga KMC mabao 6-1, KMC pia waliichapa Singida BS mabao 2-0 hapo KMC Complex
Hivyo ni mchezo utakaozikutanisha timu 'zilizojisahihisha' baada ya kutofanya vizuri katika mechi zilizotangulia
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi anakwenda kukabiliana na waliokuwa waajiri wake ambao alidumu nao kwa takribani siku 36
Yanga imekuwa na rekodi ya kibabe katika dimba la KMC Complex, ni wazi Singida BS watakumbana na aina tofauti ya soka kulinganisha na vile walivyocheza mara ya mwisho Zanzibar
Mchezo mwingine unaopigww jioni ya leo ni kati ya Fountain Gate dhidi ya Tabora United uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara