Local,Normal News,Azam, Simba

Simba, Azam Fc kuonyeshana kazi kwa Mkapa leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Feb 2025
Simba, Azam Fc kuonyeshana kazi kwa Mkapa leo

Kikosi cha Simba leo kinahamishia mawindo yake katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam Fc kwenye mwendelezo wa ligi kuu ya NBC

Ni Mzizima Derby, moja ya mechi ngumu ambayo matokeo yake yanaweza kuiweka Simba katika nafasi nzuri kwenye mbio za ubingwa au kuvuruga hesabu ingawa bado ni mapema kwa sababu kuna mechi nyingi za kuchezwa

Hata hivyo Azam Fc ni miongoni mwa timu shindani katika mbio za ubingwa hivyo kama Simba itachukua alama tatu dhidi yao ni wazi zitakuwa na thamani kubwa

Licha ya Simba kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa visiwani Zanzibar, takwimu zinaonyesha mechi kati ya Simba dhidi ya Azam Fc haijawahi kuwa nyepesi

Simba imekuwa na msimu bora mpaka sasa, ikifanya vizuri ligi ya ndani na Kimataifa, bado inaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi leo

Baada ya kukosa ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, leo Azam Fc inahitaji kushinda ili kuweka hai malengo yao katika mbio za ubingwa

Ni wazi kama Azam Fc itafungwa leo, pengine watahitaji kubadili malengo yao ya msimu huu kwani haitakuwa rahisi kwao tena kuwa bingwa

Sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 43 wakati Yanga iko kileleni ikiwa na alama 55 huku Simba ikishika nafasi ya pili ikiwa na alama 50

Baada ya mechi ya leo Azam Fc watasalia na mechi 9 wakati Simba itakuwa na mechi 10

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’