Medo atua Singida BS

Joel JJ By Joel JJ β€’ 25th February 2025


Medo atua Singida BS

Klabu ya Singida Black Stars imetangaza kumuongeza Melis Medo kama kocha msaidizi na mshauri wa benchi la ufundi wa timu hiyo

Medo aliyeachana na Kagera Sugar hivi karibuni, atashirikiana na makocha Juan Magro, Muhibu Kanu chini ya kocha mkuu David Ouma

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Singida BS mapema leo, mabadiliko hayo ni muendelezo wa marekebisho kwenye benchi lao la ufundi

Hivi karibuni Singida Black Stars walimuongeza Juan Magro kama kocha msaidizi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.