Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba jana
Licha ya ushindi huo, Hamdi amesema wachezaji wake walipata wakati mgumu kukabiliana na hali ya eneo la kuchezea la uwanja wa CCM Kirumba
"Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu muhimu lakini niseme wazi, uwanja haukuwa rafiki upande wetu"
"Ukiwa mbali unaweza kudhani uwanja huu uko katika hali bora lakini nikwambie haikuwa rahisi hata kutuliza mpira"
"Utaona kipindi cha kwanza wachezaji wangu walipata wakati mgumu lakini nafurahi kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko tulitulia na tumeweza kupata ushindi"
"Alama tatu za mchezo huu ni muhimu sana kwetu katika kukamilisha malengo yetu. Niwapongeze mashabiki wa Yanga waliokuja kwa wingi uwanjani kutuunga mkono. Mashabiki wameendelea kunishangaza niwapongeze kwa kile wanachofanya kwa timu yao," alisema Hamdi
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa Stephane Aziz Ki aliyepachika mabao mawili na Chadrack Boka aliyefunga bao lake kupitia mpira wa faulo