Simba yaichapa Coastal Union 3-0

Joel JJ By Joel JJ β€’ 1st March 2025


Simba yaichapa Coastal Union 3-0

Mnyama Simba ameunguruma dimba la Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Steven Mukwala ndiye aliyekuwa shujaa wa Simba katika mchezo huo akiweka hat-trik yake ya kwanza msimu ikiwa pia ni hat-trik ya kwanza kutoka kwa klabu ya Simba

Mukwala alihesabu bao la kwanza dakika ya 30 akimalizia pasi murua kutoka kwa David Kameta 'Duchu' aliyeanza leo

Wakati mchezo huo ukiwa dakika za lala salama kuelekea mapumziko, Elie Mpanzu akatngeneza assist yake ya tatu msimu huu akimuwekea Mpanzu kuandikisha bao lake la pili

Simba iliendelea kutawala mchezo huo hata baada ya mapumziko na alikuwa ni Mukwala tena aliyefunga bao la tatu akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango wa Coastal Union baada ya shuti la Mpanzu

Mukwala sasa amefikisha mabao nane akimfikia mshambuliaji mwenzake Lionel Ateba sasa Mukwala akionekana kuitaka nafasi katika kikosi cha kwanza

Leo wachezaji wa Simba walionekana kuwa na ari na kiu ya kushinda mchezo huo pengine Mnyama alistahili kuondoka na ushindi mnono zaidi kwa kuzingatia idadi ya nafasi zilizotengenezwa

Alama tatu muhimu ambazo zinaifanya Simba ifikishe alama 54, alama nne nyuma ya watani zao Yanga wenye alama 58 huku Simba ikiwa na mechi moja ya kiporo

Simba sasa inahitaji kushinda mchezo unaofuata dhidi ya Yanga March 08 ili kuwa katika nafasi nzuri ya kurejea kileleni


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.