Local,Normal News,Yanga

Hatuihofii Simba - Hamdi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Mar 2025
Hatuihofii Simba - Hamdi

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa saa 1:15 usiku, Hamdi amesema anaiheshimu klabu ya Simba na hii ni mechi kubwa lakini anaamini ubora wa timu yake unakwenda kuamua mchezo huo

"Nafurahi kuwa hapa na klabu ya Yanga na zaidi kucheza mechi hii ya derby katika miongoni mwa mechi kubwa Afrika. Hii haitakuwa mara ya kwanza kushiriki mchezo mkubwa wa aina hii lakini kwa hapa Tanzania hii ni derby yangu ya kwanza na matarajio yangu ni kupata ushindi"

"Tunajua kesho ni mechi ya kipekee kulinganisha na mechi nyingine. Nafurahi nimepata siku tano za kuiandaa timu yangu kuelekea mchezo huu. Jambo muhimu ni kuwa tumefanya maandalizi mazuri na tunaamini mechi hii mchezo wa mpira wa miguu utashinda"

"Natarajia kuona mchezo wa wazi kila timu ikijaribu kushinda, tunapaswa kuwa bora kimbinu na kutumia vyema nafasi tutakazotengeneza. Najua Simba ni timu imara, nimesema lazima tuwe bora kimbinu, tumeandaa mazingira yote ya mchezo naamini tutafanya kitu kizuri," alisema Hamdi

Hamdi amesisitiza hana hofu yoyote kuelekea mchezo huo kwani anaamini uwezo wa timu yake na zaidi mchezo wa mpira wa miguu ni burudani

"Kama kocha sina wasiwasi wowote kuelekea mchezo huu, sisi ni Yanga, timu kubwa Afrika hatuwezi kuhofia mechi hii. Naamini wachezaji wangu watapambana ili kuwapa furaha mashabiki wetu," alisema Hamdi

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’