Local,Normal News,Yanga, Simba

Mechi ya Yanga dhidi ya Simba itachezwa - TPLB

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Mar 2025
Mechi ya Yanga dhidi ya Simba itachezwa - TPLB

Sakata la Simba kugomea mchezo dhidi ya watani wao, Yanga, limechukua sura mpya baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutoa tamko kwamba mechi hiyo ipo palepale kama ilivyopangwa

Simba ilitoa tamko usiku wa kuamkia leo ikisema haitaleta timu uwanjani kwenye mchezo huo kufuatia msafara wa kikosi chake kuzuiwa jana usiku kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambao ndio utatumika kwenye mechi hiyo

Simba ilizuiwa na kundi la watu wanaodhaniwa ni mashabiki wa Yanga maarufu kwa jina la makomandoo, huku pia ikimtaja meneja wa uwanja kudai hakuwa na taarifa kwamba Wekundu hao watakwenda kufanya mazoezi uwanjani hapo

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Steven Mnguto amesema licha ya Simba kudai haitaleta timu mchezo huo upo palepale huku akiwataka mashabiki waliokata tiketi kujipanga kwenda uwanjani

"Matukio yote tumeyasikia na tunayafuatilia kuanzia hatua ambayo yalijiri, kuna ripoti za awali tumeshazipokea kwa wasimamizi mbalimbali na tunazifanyia kazi," amesema Mnguto

"Kwanza niwatoe wasiwasi mashabiki wa soka na wadau kwa ujumla. Mchezo upo palepale kama ambavyo kalenda yetu ya soka inavyosema, hakuna mabadiliko yoyote, mashabiki wajipange kuja kutazama mchezo"

Mnguto ameongeza kuwa kufuatia taarifa hiyo ya Simba ameitisha kikao cha dharura cha kamati ya usimamizi wa ligi kitakachojadili tukio lililotokea jana usiku

"Nimeitisha hiki kikao cha haraka kitafanyika asubuhi hii. Bahati mbaya sitaweza kushiriki, lakini nimemuagiza makamu wangu akisimamie tujadili matukio haya yaliyotokea jana na hii taarifa ya Simba," amesema Mnguto

"Tutatoa taarifa kamili mapema sana kwenda kwa wadau wote. Kwa hiyo tunaomba watu wawe na subira, lakini kama nilivyosema mchezo upo kama ambavyo umepangwa hakuna mabadiliko. Hayo mengine tutayatolea ufafanuzi zaidi mara baada ya kikao kukamilika"

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’