Kufuatia mfululizo wa matukio ambayo yalipelekea klabu ya Simba kushindwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa jana, Bodi ya Ligi imetangaza kuahirishwa mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao ulipaswa kupigwa leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Taarifa iliyotolewa na Bodi mapema leo imebainisha kuwa kwa sasa Kamati inapitia ushahidi mbalimbali wa matukio yaliyojiri jana usiku kabla ya kutoa maamuzi ya kilichojitokeza
Aidha Bodi imetangaza kuahirisha mchezo huo na sasa utapangiwa tarehe nyingine
Simba ilitangaza msimamo wake mapema kutoshiriki mchezo huo hadi pale wale walioihujumu Simba kuchukuliwa hatua




