International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu March 10 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Mar 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu March 10 2025

Chelsea wanapanga kutoa ofa kwa kiungo wa kati wa Sunderland Muingereza Jobe Bellingham, 19. (Sun via Metro)

Manchester City wanazungumza na wawakilishi wa mchezaji wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz wakati wakiangalia uwezekano wa kumnunua winga huyo wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka 21. (Football Insider)

Real Madrid na Bayern Munich pia wana nia ya kumsajili Wirtz, ambaye huenda akaondoka Bayer Leverkusen msimu huu wa joto. (Mundo Deportivo)

Chelsea na Barcelona zimeonesha nia thabiti ya kutaka kumsajili winga wa Ureno Rafael Leao, 25, kutoka AC Milan. (Calciomercato)

Manchester City wanafikiria kutoa ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Crystal Palace na Uingereza Adam Wharton, 21. (TBR Football)

Beki wa kati wa England Jarrad Branthwaite anaweza kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Everton kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atadai kandarasi ya takribani pauni 150,000 kwa wiki ili kusalia katika klabu hiyo. (Football Insider)

Everton itahitaji kulipa pauni milioni 40 kumsajili beki wa kati wa Ecuador Joel Ordonez, 20, kutoka Club Brugge msimu wa joto. (Football Insider)

Arsenal, Liverpool na Chelsea zimekuwa zikimfuatilia mshambuliaji wa Inter Milan Mfaransa Marcus Thuram, 27. (TBR Football) Bayern Munich wamekusanya taarifa kuhusu mchezaji wa Bournemouth Dean Huijsen ingawa beki huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 19 bado hajawa lengo mahususi msimu huu wa joto. (Florian Plettenberg)

Deportivo La Coruna inahofia kumuuza winga wa Uhispania Yeremay Hernandez iwapo watakosa kupandishwa daraja kwenye La Liga kwani kipengele chake cha kuachiliwa msimu wa joto kitakuwa takribani euro milioni 35 (Β£29.4m) na vilabu kama Chelsea, Napoli na Como vilikaribia kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 mwezi Januari. (AS -in Spanish)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, 30, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Bayern Munich hadi 2029. (Fabrizio Romano)

Juventus wanataka kukubali mkataba mwingine wa mkopo kwa Randal Kolo Muani msimu wa joto na kujumuisha chaguo la kumnunua mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 26, kutoka Paris St-Germain. (Calciomercato)

Barcelona wameanza mazungumzo ya kuongeza mkataba wa mlinda lango wa Poland Wojciech Szczesny mwenye umri wa miaka 34. (Nicolo Schira)

Mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Atletico Madrid, Andrea Berta amekubali kuchukua nafasi hiyo hiyo katika klabu ya Arsenal, licha ya kutakiwa na vilabu vya Manchester United na Paris St-Germain. (Sky Sports)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’