International,Transfer News,

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu March 17 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Mar 2025
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu March 17 2025

Manchester United wametoa ofa ya euro 70m (Β£58.9m) ili kumsajili mshambuliaji wa Brazil Raphinha, 28, kutoka Barcelona katika majira ya msimu wa joto. (Fichajes.net)

Manchester City italazimika kulipa angalau pauni milioni 70 ikiwa inataka kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 22, kutoka Real Madrid. (Football Insider)

Newcastle wanataka kumbakisha mshambuliaji wa Msweden Alexander Isak katika klabu hiyo lakini wanafuatilia kwa karibu wachezaji kadhaa, akiwemo mshambuliaji chipukizi wa Ipswich, Muingereza Liam Delap, 22, na Msweden wa Sporting Viktor Gyokeres, 26, kama wachezaji wanaotarajiwa kuchukua nafasi yake ikiwa Isak ataondoka huku kukiwa na ripoti ya kutakiwa na Liverpool. (Teamtalk)

Mshambulizi wa zamani wa Marekani na Chelsea Christian Pulisic, 26, yuko kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na klabu ya Italia AC Milan. (ESPN)

Arsenal na Chelsea zinaonekana kuwa mbele ya Liverpool katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Ufaransa Marcus Thuram, 27, ambaye anaripotiwa kuwa na kipengele cha kuuzwa kwa pauni milioni 71. (Football Insider)

Mshambulizi wa Napoli Victor Osimhen, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray, huenda akahamia Ligi kuu ya England msimu ujao, anasema mchezaji mwenzake wa Nigeria William Troost-Ekong. (Talksport)

Tottenham Hotspur ni moja ya klabu kadhaa vya ligi kuu England zinazofuatilia maendeleo ya kiungo wa kati wa Inter Miami, Mmarekani Benjamin Cremaschi, 20. (TBR Football)

AC Milan imetuma wasaka vipaji wake kumtazama mlinzi wa Burnley Maxime Esteve, 22, huku Everton na West Ham pia zikimtaka Mfaransa huyo. (Alan Nixon)

Arsenal wanafikiria kumnunua mlinzi wa kushoto wa Ajax Mholanzi Jorrel Hato, 19, licha ya kuibuka kwa Myles Lewis-Skelly msimu huu (TBR Football)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’