Local,Normal News,Simba

Chamou aahidi kuziba pengo la Che Malone Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Mar 2025
Chamou aahidi kuziba pengo la Che Malone Simba

Wakati hatma ya beki kisiki Che Fondoh Malone ikiwa bado mikononi mwa madaktari wanaomtibu, beki aliyeziba nafasi yake Chamou Karaboue amesema hakuna kitakachoharibika kwani yeye na Abdulrazak Hamza wataendelea kuilinda ngome ya Simba

Che Fondoh alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Azam Fc, kuna taarifa kuwa aina ya majeraha ambayo yanamkabili Che Fondoh, huenda yakamuweka nje kwa muda mrefu zaidi kinyume na vile ilivyotarajiwa

Chamou amesema sasa ameshaizoea ligi kuu ya NBC na hivyo anafahamu vyema jinsi ya kukabiliana na washambuliaji wa timu pinzani

Amesema maelewano na Abdulrazack Hamza ni mazuri kwani muda mwingi aliokuwa akipata nafasi alicheza nae na hata Che Malone, hivyo alihitaji muda wa kumuelewa zaidi na ameupata.

"Ukuta wetu upo imara kuhakikisha hatutoki kwenye njia ya malengo yetu tuliyojiwekea, nacheza kwa maelewano mazuri na mabeki wenzangu kwa sababu nimeshawasoma"

"Ukizingatia viungo wetu wa juu ni watu wanaojua kutupunguzia presha hivyo nataka kutumia mechi hizi ambazo Che Malone hatakuwepo uwanjani kuthibitisha kwamba mimi ni beki sahihi kuitumikia Simba," alisema ChamouΒ 

Tangu Che Malone apate majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Chamou, Simba imecheza mechi tatu na kushinda zote pasipo kuruhusu bao

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’