Jumatatu ijayo, March 24 2025 klabu ya Singida Black Stars inatarajiwa kuzindua uwanja wake mpya huku ikiwaalika mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga katika uzinduzi huo
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya mapumziko ya takribani siku sita, kikosi cha Yanga kitarejea mazoezini Jumatano, kujiandaa na mchezo huo pamoja na mechi nyingine zinazofuata
"Baada ya mchezo wetu wa kombe la FA dhidi ya Coastal Union, uongozi ulitoa siku sita za mapumziko kwa wachezaji"
"Timu inatarajiwa kurejea mazoezini siku ya Jumatano kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kirafiki dhidi ya Singida Black Stars na mechi za kuhitimisha msimu"
"Wachezaji wote ambao hawako katika majukumu ya timu za Taifa watarejea mazoezini chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Miloud Hamdi," alisema
March 29 Yanga itacheza mechi ya hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Songea Unted na kisha kuivaa Tabora United katika mchezo wa ligi kuu April 1 uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora