Beki wa Liverpool Virgil van Dijk amesema haogopi kuhusu mustakabali wake wa kuendelea kubakia Liverpool huku nahodha huyo wa Reds akikiri kuwa yuko tayari endapo hataendelea kusalia klabuni hapo baada ya mwisho wa msimu
Mkataba wa sasa wa Van Dijk unamalizika Juni na mazungumzo na Liverpool bado yanasuasua
Beki huyo mwenye umri wa miaka 33, aliyekuwa na mafanikio kwa miaka saba Anfield, atafikia kikomo ikiwa hakuna mkataba mpya utakaosainiwa
Van Dijk, ambaye jana aliiongoza Liverpool katika fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Newcastle na kukubali kipigo cha mabao 2-1, katika Uwanja wa Wembley, hajaficha nia yake ya kusalia Merseyside
"Sitaki kuleta wasiwasi wowote , ninaweka kichwa changu chini na kuangazia kwa matumaini kushinda michezo 10 ijayo. Nina uhakika ifikapo mwisho wa msimu kutakuwa na habari njema, lakini ni aina gani ya habari sina uhakika," alisema