International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano, March 19 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Mar 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano, March 19 2025

Klabu ya Saudia Al-Nassr inapanga kutoa ofa ya kumnunua beki wa kati wa Arsenal na Brazil Gabriel Magalhaes, 27 msimu wa joto. (GiveMeSport)

Real Madrid wataongeza dau lao la kumsajili beki Dean Huijsen mwenye umri wa miaka 19 kutoka Bournemouth msimu huu wa joto baada ya kupandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Uhispania. (Sun)

Bournemouth wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mlinda mlango wa Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 26, kutoka Liverpool. (Sportsport)

Newcastle United wanatayarisha ofa ya mkataba mpya ambao utaongeza maradfu mshahara wa mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, (GiveMeSport)

Napoli watajaribu kumnunua mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund msimu huu wa joto, lakini hawawezi kumudu bei inayotakiwa na Manchester United ya Β£50m. (Gazzetta dello Sport)

Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray, anaweza kwenda Manchester United kama sehemu ya mkataba wa Hojlund kwenda Napoli (Mirro)

Chelsea wanafikiria kulipa ada ya adhabu ili kukwepa jukumu la kumnunua moja kwa moja kwa pauni milioni 25 kiungo Jadon Sancho msimu huu wa joto, ambaye yuko hapo kwa mkopo akitokea Manchester United. (The i paper)

Mkurugenzi mpya wa michezo mtarajiwa wa Arsenal Andrea Berta anavutiwa na mshambuliaji wa Wolves raia wa Brazil Matheus Cunha, ambaye ana kipengele katika mkataba wake cha kuuzwa kwa Β£62.5m. (Teamtalk)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 22, yuko tayari kujiunga na Manchester City msimu huu wa joto huku kukiwa na wasiwasi kuhusu nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid. (Football Insider)

Kocha mkuu Unai Emery anaishinikiza timu yake ya Aston Villa kumsajili kw auhamisho wa kudumu mshambuliaji wa Hispania Marco Asensio, 29, anayetoka kwa mkopo Paris St-Germain. (GiveMeSport)

Arsenal wanafuatilia kwa karibu masuala ya mkataba wa Leroy Sane huko Bayern Munich kwani winga huyo wa Ujerumani, 29, anaweza kupatikana kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, ni mmoja wa wachezaji ambao Manchester United wako tayari kuwauza msimu huu wa joto ili kuongeza bajeti yao ya uhamisho. (Florian Plettenberg)

Winga wa Ureno Bernardo Silva, 30, anatarajia kusalia Manchester City msimu huu wa joto ili kumalizia mkataba wake. (Mirror)

Tottenham ni moja ya vilabu kadhaa vinavyovutiwa na kiungo wa kati wa Inter Miami Mmarekani Benjamin Cremaschi, 20, ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaopendwa sana na Lionel Messi (Teamtalk)

Barcelona wanataka kumuuza Ansu Fati, 22 msimu huu wa joto, ingawa winga huyo wa Hispania, alikataa kuuzwa katika dirisha lililopita la Januari. (Fabrizio Romano)

Manchester United ni moja ya vilabu kadhaa vya ligi kuu England vinavyofikiria kumnunua kiungo wa kati wa Sunderland Jobe Bellingham mwenye umri wa miaka 19. (Teamtalk)

Crystal Palace wanapanga mpango wa kumsajili mshambuliaji Muingereza Hayden Hackney mwenye umri wa miaka 22 kutoka Middlesbrough msimu huu wa joto. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’