Local,Normal News,Simba

Kocha Simba matumaini kibao CAF CC

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Mar 2025
Kocha Simba matumaini kibao CAF CC

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids ana matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ambapo mechi ya mkondo wa kwanza itapigwa April 02 huko Misri na marudiano kupigwa dimba la Benjamin Mkapa April 09

Fadlu amesema kikosi chake sasa kimeimarika tofauti na walivyoanza msimu, wanajua watakabiliwa na mechi ngumu Misri lakini watahitaji kupambana na muhimu angalau wafunge bao la ugenini

"Tutakwenda Misri huku tukifahamu haitakuwa mechi nyepesi ugenini lakini nafurahi kuona wachezaji wangu sasa wako tayari na wanafahamu mazingira ambayo tutakutana nayo"

"Tuna timu changa yenye wachezaji wengi ambao hawana uzoefu na michuano ya Kimataifa, lakini mechi za hatua ya awali na makundi zimesaidia kuwaimarisha kwa kiasi kikubwa"

"Kumaliza nafasi ya kwanza katika hatua ya makundi ni jambo kubwa ambalo limetuongezea kujiamini kuelekea hatua hii inayofuata"

"Tutapaswa kucheza kwa umakini mkubwa ugenini ili tuwe na nafasi ya kusonga mbele katika mechi ya pili tutakayocheza nyumbani. Malengo yetu ni kuona tunafika mbali katika michuano hii," alisema Fadlu

Aidha Fadlu amebainisha kuwa mafanikio ya timu yake hayapaswi kutegemea mchezaji mmoja, kila mchezaji katika kikosi chake ana umuhimuΒ 

Amesema ili kufanya vizuri katika michuano yote wanayoshiriki, ni lazima kuwa na kikosi kipana ambacho kitatoa nafasi kwa kila mchezaji

"Wakati niko Orlando Pirates, tulicheza fainali ya kombe la Shirikisho 2022/23 lakini hatukuwa na kikosi kipana, tulitumia wachezaji walewale katika kila mechi"

"Hili ilitusumbua sana kwenye ligi baada ya michuano ya CAF kumalizika, kama tunataka kufanya vizuri katika mashindano yote lazima tuwe na uwiano mzuri kitimu"

"Kila mchezaji hapa ana nafasi ya kuchangia mafanikio ya timu na sio kutegemea mchezaji mmoja," aliongeza Fadlu

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’