Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema kikosi kinaendelea na maandalizi kabambe kuelekea mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Bigman Fc ambao utapigwa Alhamisi March 27 katika uwanja wa KMC Complex
Ahmed amesema Simba inafanya maandalizi ya mechi mbili, wakati wakijifua kuikabili Bigman Fc, pia wanajiandaa kwa mchezo wa kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC) dhidi ya AL Masry utakaopigwa April 02 huko Misri
Ahmed amesema mchezo dhidi ya Bigman Fc ni muhimu sana kwao na wamejipanga kucheza mechi yenye ushindani
"Kikosi kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa kombe la FA dhidi ya Bigman Fc ambao utapigwa Alhamisi, katika uwanja wa KMC Complex"
"Mechi hii ni muhimu sana kwetu, na itakuwa sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa CAF dhidi ya Al Masry utakaopigwa wiki ijayo"
"Wachezaji wote wako tayari kwa mechi ya kiushindani dhidi ya Bigman Fc, sisi hatuwadharau wapinzani wetu kwani tunajua kufuzu hatua ya 16 katika michuano hii ya FA sio jambo jepesi"
"Tunaamini ni timu nzuri ya lazima tujiandae vyema kukabiliana nao ili tuweze kushinda na kusonga mbele hatua inayofuata katika michuano hii," alisema Ahmed
Bigman Fc ni timu inayoshiriki ligi ya Championship kwa sasa. Timu hii zamani ilikuwa ikiitwa Mwadui Fc