Baada ya kujihakikishia tiketi ya kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Songea United, kikosi cha Yanga kinaelekeza nguvu zake kwenye ligi kuu ya NBC
Jumanne, April 01 Yanga itaondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Tabora wanakokabiliwa na mchezo dhidi ya Tabora United utakaopigwa Jumatano katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanakwenda Tabora wakiwa dhamira ya kulipa kisasi dhidi ya walina asali hao ambao mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam walipata ushindi wa mabao 3-1 dimba la Azam Complex
Kamwe ni miongoni mwa maafisa wa Yanga waliotangulia Tabora kuwahamasisha mashabiki wao kuelekea mchezo huo
Kamwe amesema wanaichukulia mechi hhii kama fainali na hakuna matokeo zaidi ya ushindi ambayo Wananchi watahitaji