International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili March 30 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Mar 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili March 30 2025

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ureno Bruno Fernandes, 30, analengwa na Real Madrid kwa pauni milioni 90. (Star)

Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal anayekuja, Andrea Berta atakuwa na kibarua cha kukamilisha dili la kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi huku kukiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Real Madrid. (Mirror)

Manchester City inamtazama mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Pedri kama chaguo bora kwa safu yao ya kiungo lakini Barcelona hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Fichajes – In Spanish)

Manchester City wamefanya mazungumzo ya mapema kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Sweden Hugo Larsson, 20, huku Eintracht Frankfurt wakishikilia kwa angalau pauni milioni 50. (Sky Sports Germany)

Chelsea wamemfanya mlinzi wa Barcelona Mfaransa Jules Kounde, 26, kuwa lengo lao kuu katika dirisha la majira ya joto. (Sport – In Spanish)

Barca wanakaribia kuafikiana kuongezewa mkataba kwa kipa wa Poland Wojciech Szczesny mwenye umri wa miaka 34 hadi Juni 2026. (Fabrizio Romano)

Bournemouth wanataka kumsajili mlinda lango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga kwa mkataba wa kudumu kutoka Chelsea msimu huu wa joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa yuko kwa mkopo wa msimu mzima na Cherries. (Fabrizio Romano)

Atletico Madrid wanamtaka kiungo wa kati wa Chelsea na Argentina Enzo Fernandez, 24 - huku timu hiyo ya Uhispania ikitayarisha ofa ya takriban Β£25m, pamoja na kiungo wa kati wa Uhispania Pablo Barrios, 21, aliyeshinda Kombe la Dunia. (Fichajes – In Spanish)

RB Leipzig wana nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Sunderland Jobe Bellingham, 19, lakini fikiria bei ya Paka Weusi wanaomtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa U21 wa Uingereza kuwa juu mno. (Sky Sport Germany)

Kocha wa akademi ya Manchester United Colin Little anasema fowadi wa Uingereza Cole Palmer alikaribia kujiunga na klabu hiyo ya Old Trafford kutoka Manchester City alipokuwa na umri wa miaka 16. Palmer, 22, alibaki City lakini akaondoka na kujiunga na Chelsea mwaka jana. (Metro)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’