Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kumshikilia Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe kwa tuhuma za kuwachafua viongozi wa Serikali
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao amethibitisha kwamba, Kamwe anashikiliwa tangu Jana usiku, kwa tuhuma hizo. Abwao amesema bado Kamwe yuko kizuizini akiendelea na mahojiano juu ya tuhuma hizo ambapo taarifa zaidi zitatolewa baadaye





