Yanga imebeba alama zote tatu uwanja wa KMC Complex ikiibukaa na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Bao la dakika ya 34 lililofungwa Pacome Zouzoua akimalizia krosi ya Maxi Nzengeli lilitosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu ambazo zinawafanye wajiimarishe kileleni kwa tofauti ya alama 7 baada ya kufikisha alama 64
Ni mchezo ambao pengine Yanga ingeweza kupata ushindi mnono zaidi lakini mlinda lango wa Coastal Union alikuwa kikwazo kwao
Pacome ameendelea kutamba akifunga bao lake la nane msimu huu huku Nzengeli nae akiongeza asisti ya nane