International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne April 08 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Apr 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne April 08 2025

Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Wolves na Brazil Matheus Cunha, 25, ambaye kifungu cha kuachiliwa kwake cha pauni milioni 62.5 kitaanza kutumika msimu huu. (Talk sport)

Tottenham Hotspur haitamsajili mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 29, kwa uhamisho wa kudumu mara tu mkataba wake wa mkopo utakapokamilika msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Chelsea hawana nia tena ya kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, msimu huu. (CaughtOffside)

Inter Miami wanapanga kumpa kandarasi kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa timu za Saudi Arabia. (Mirror)

Winga wa chini ya miaka 21 wa England Jamie Gittens, 20, anataka kuondoka Borussia Dortmund msimu huu wa joto. Vilabu kadhaa vya Ligi Kuu vinavutiwa naye. (Sky Germany)

Everton na Brighton wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ipswich na England U21 Liam Delap, 22, ambaye kifungu chake cha pauni milioni 40 kitaanza kutumika iwapo Ipswich itashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (TeamTalk)

Fiorentina itawezesha kuongeza mwaka mmoja katika kandarasi ya mlinda mlango wa Uhispania David de Gea, 34, na kumbakisha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United hadi Juni 2026. (Fabrizio Romano)

Leicester City wanatazamia kumtimua meneja Ruud van Nistelrooy baada ya kushindwa mara tisa mfululizo. (Football Insider)

Bayer Leverkusen wanavutiwa na mlinda mlango wa Brentford na Uholanzi Mark Flekken, 31, huku Bees wakitaka takribani euro 15m (Β£12.8m). (Sky Germany)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’