Katika kilele cha burudani ya soka barani Afrika, jana Klabu ya Simba ya Tanzania iliandika historia nyingine kwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-1 dhidi ya Al Masry ya Misri, katika mchezo wa marudiano uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 2-0 ndani ya dakika 90, na hivyo kusawazisha matokeo ya jumla kuwa 2-2, baada ya kupoteza kwa idadi hiyo ya mabao katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Misri
Hatimaye, mikwaju ya penati iliihukumu Al Masry na kuiwezesha Simba kutinga hatua ya nne bora na sasa inawania rekodi ya kucheza fainali ya michuano hiyo kama walivyofanya mwaka 1993
Kutokana na mafanikio hayo makubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, alituma salamu za pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi, na mashabiki wa Simba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter)
βPongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika Nusu Fainali,β ulisomeka ujumbe wa Mh Rais
Kupitia bonas ya goli la Mama katika michuano hiyo, klabu ya Simba ilivuna kitita cha Tsh Milioni 30 baada ya ushindi huo dhidi ya Al Masry
Simba ilifunga mabao mawili katika dakika 90 na pia kuibuka kidedea kwenye mikwaju ya penati