Local,Normal News,Simba

Rais Samia aipongeza Simba kwa kufuzu nusu fainali CAF CC

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Apr 2025
Rais Samia aipongeza Simba kwa kufuzu nusu fainali CAF CC

Katika kilele cha burudani ya soka barani Afrika, jana Klabu ya Simba ya Tanzania iliandika historia nyingine kwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-1 dhidi ya Al Masry ya Misri, katika mchezo wa marudiano uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 2-0 ndani ya dakika 90, na hivyo kusawazisha matokeo ya jumla kuwa 2-2, baada ya kupoteza kwa idadi hiyo ya mabao katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Misri

Hatimaye, mikwaju ya penati iliihukumu Al Masry na kuiwezesha Simba kutinga hatua ya nne bora na sasa inawania rekodi ya kucheza fainali ya michuano hiyo kama walivyofanya mwaka 1993

Kutokana na mafanikio hayo makubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, alituma salamu za pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi, na mashabiki wa Simba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter)

β€œPongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika Nusu Fainali,” ulisomeka ujumbe wa Mh Rais

Kupitia bonas ya goli la Mama katika michuano hiyo, klabu ya Simba ilivuna kitita cha Tsh Milioni 30 baada ya ushindi huo dhidi ya Al Masry

Simba ilifunga mabao mawili katika dakika 90 na pia kuibuka kidedea kwenye mikwaju ya penati

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’