Local,Normal News,Yanga, Azam

Azam Fc yakubali kichapo mbele ya Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Apr 2025
Azam Fc yakubali kichapo mbele ya Yanga

Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuichapa Azam Fc mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi ikionyesha dhamira ya kusaka ushindi mapema na alikuwa Pacome Zouzoua aliyefunga bao la kwanza dakika ya 11 akimalizia kazi ya Prince Dube

Mabingwa hao watetezi waliendelea kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza wakitengeneza nafasi nyingi lakini mlinda lango wa Azam Fc Zuberi Foba alikuwa kikwazo akiokoa michomo ya hatari

Alikuwa ni Prince Dube aliyewaadhibu waajiri wake hao wa zamani akifunga bao la pili dakika ya 34 akimalizia pasi ya Mudathir Yahya

Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa na uongozi wa mabao 2-0. Kipindi cha pili Wananchi waliendelea kutawala mchezo lakini wakati mchezo ukielekea ukiongoni kasi yao ilipungua na kuwapa nafasi Azam Fc kurejea mchezoni

Lusajo Mwaikenda akafunga bao la kufutia machozi kwa upande wa Azam Fc akimalizia kona ya Feisal Salum

Hata hivyo Wananchi walifanikiwa kulinda uongozi wao hadi pale mwamuzi Ahmed Arajiga alipomaliza mchezo

Yanga imefikisha alama 67 sasa ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama 10 huku ikisaliwa na mechi nne tu kuhitimisha msimu

Ni ushindi muhimu kwa Yanga ambao kwa hakika unawaweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa

Aidha ushindi huo unaihakikishia Yanga kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao kwani Wananchi sasa wana uhakika wa kumaliza nafasi mbili za juu

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
3h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
4h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
5h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
6h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
6h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’