Klabu ya Simba itatumia uwanja wa New Amaan Complex katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumapili April 20, saa 10 jioni
Imeelezwa uwanja wa Benjamin Mkapa ambao mchezo huo ulipaswa kupigwa bado uko katika maboresho ya eneo la kuchezea 'pitch'
Uwanja wa Amaan ulipitishwa CAF kutumika katika mashindano ya Shirikisho hilo baada ya kufanyiwa maboresho
Eneo lake la kucheza lilifanyiwa maboresho makubwa kwa kuondoa nyasi bandia na kupanda nyasi asili




