International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, April 15 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Apr 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, April 15 2025

Arsenal wamewasiliana na Bayern Munich kuulizia upatikanaji wa winga Kingsley Coman, mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports)

Eintracht Frankfurt wanataka ada ya takriban €100milioni (Β£86.3m) kwa mshambuliaji Hugo Ekitike, mwenye umri wa miaka 22, huku Arsenal na Tottenham wakionyesha nia ya kumsajili. (Bild - in German)

Tottenham wako tayari kuvunja rekodi yao ya usajili na kulipa takriban Β£65m kumsajili mshambuliaji wa Wolves Matheus Cunha, mwenye umri wa miaka 25. (Fichajes - in Spanish)

Crystal Palace wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 27, kufuatia mafanikio yake kwa mkopo akiwa Aston Villa. (Sun)

Liverpool na Everton wanatarajiwa kushindana kumsajili kiungo wa Sunderland Chris Rigg, mwenye umri wa miaka 17, majira ya kiangazi. (The i)

Manchester United hawatarajiwi kumuuzia kipa Andre Onana, mwenye umri wa miaka 29, majira haya ya joto isipokuwa kama dau kubwa la faida kutokana na ada ya Β£47m waliyolipa litawekwa mezani (NBC Sports)

Hata hivyo, United wamepunguza bei ya kumuuza mshambuliaji Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 20, kutoka zaidi ya Β£50m hadi chini ya Β£40m ili kurahisisha mauzo. (Tutto Mercato Web)

United wanaonyesha nia ya kumsajili kijana wa Ajax Abdellah Ouazane, mwenye umri wa miaka 16, baada ya kung'ara akiwa Morocco kwenye mashindano ya U17 Africa Cup of Nations. (Daily Mail)

Manchester City watamuongeza mkataba wa mwaka mmoja kiungo Ilkay Gundogan, mwenye umri wa miaka 34, na kumbakiza hadi mwaka 2026. (Fabrizio Romano)

Real Madrid watajaribu kumsajili mshambuliaji wa City Erling Haaland, mwenye umri wa miaka 24, iwapo Vinicius Jr ataondoka na kuelekea Saudi Arabia kama inavyodaiwa. (Sky Sports)

Barcelona wameweka dau la thamani ya Β£78m kwa winga Raphinha, mwenye umri wa miaka 28, kufuatia uvumi wa kuvutiwa na klabu za Saudi Pro League. (Catalunya Radio)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’