Klabu ya JKT Tanzania na Singida Black Stars jana ziliunga na Simba kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kushinda mechi za robo fainali
JKT Tanzania ikiichapa Pamba Jiji mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo huku Singida Black Stars ikiichapa Kagera Sugar mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM LITI
Timu hizo zimeunga na Simba ambayo juzi ilitangulia nusu fainali ikiichapa Mbeya City mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Leo Wananchi Yanga wao watashuka dimbani kumenyana na Stand United katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex
Kama Yanga itashinda mchezo huo, basi itatinga nusu fainali ambapo itachuana na JKT Tanzania katika mchezo ambao utapigwa dimba la KMC Complex
Singida Black Stars watachuana na Simba katika mchezo wa nusu fainali