Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Pacome Zouzoua, anakabiliwa na mapumziko ya takribani wiki mbili nje ya dimba baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC
Mchezo huo uliochezwa hivi karibuni uliisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku Zouzoua akiwa mmoja wa wafungaji na bao lingine likifungwa na Prince Dube





