Aziz Ki apiga nne Yanga ikiichapa Stand United 8-1

Joel JJ By Joel JJ β€’ 15th April 2025


Aziz Ki apiga nne Yanga ikiichapa Stand United 8-1

Yanga imetinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB kibabe kwa ushindi wa mabao 8-1 dhidi Stand United

Unaweza kusema Yanga leo ilikuwa na mazoezi ya kutengeneza nafasi ya kufunga pengine Wananchi wangeweza kufunga mabao zaidi

Baada ya majeraha ya hapa na pale, Stephane Aziz Ki leo amerejea kikosini kikamilifu akifanikiwa kufunga mabao manne huku Clatous Chama akiendeleza ubora wake akiweka kambani mabao mawil

Nickson Kibabage na Kennedy Musonda nao waliingia kambani katika mchezo huo ambao waliweka rekodi ya kufunga mabao mengi katika michuano hiyo msimu huu

Yanga sasa itachuana na JKT Tanzania katika mchezo wa nusu fainali huku watani zao Simba wakimenyana na Singida Black Stars


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.