Local,Normal News,JKT

JKT Tanzania yapania kumaliza msimu kibabe

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Apr 2025
JKT Tanzania yapania kumaliza msimu kibabe

JKT Tanzania, wapo katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakikusanya pointi 32 kupitia mechi 25, huku kocha wa timu hiyo, Ahmad Ally akipiga hesabu kali kwa mechi za tano zilizosalia ili kuhakikisha wanavuna pointi za kutosha zitakazowaacha salama

Kocha Ally alisema pointi walizonazo kwa sasa bado haziwapi dhamana ya kuendelea kusalia katika Ligi Kuu, hivyo anajipanga na wachezaji kuona kila mchezo wanautumia vyema kuvuna pointi tatu ili hadi mwisho wa msimu wasalie katika ligi kwa msimu ujao na hata kuingia 5 Bora

Akifafanua kauli iyo, kocha huyo alisema kwa hali ya sasa ni makocha kutumia mbinu kushinda mechi kuliko ufundi mwingi uwanjani ambao hautakuwa na msaada kwa kipindi hicho

Dhidi ya wapinzani iliobaki kuwakabili, raundi ya kwanza zilipokutana JKT ilifungwa 1-0 na Simba, kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Fountain Gate na 1-0Β  dhidi ya TZ Prisons, huku ikitoka suluhu na timu za Pamba Jiji na Mashujaa

"Tuna hesabu za kumaliza nafasi ya 5, ufundi upo lakini siyo jambo unaloweza ukalitegemea sana katika mechi hizi za mwisho, labda itategemea na mechi yenyewe uwe umeshinda mabao mengi, nje na hapo mchezo ukiwa mgumu lazima mbinu zitahusika zaidi,” alisema kocha Ally.

Katika mechi 25 ilizocheza hadi sasa maafande hao wameshinda michezo saba, wamepata sare 11 na kupoteza saba, wakifunga pia mabao 22 na kufungwa 21 na kumiliki pointi 32

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’